TyDiQA1.0

The Typologically Different Question Answering Dataset

Predictions

Scores

Edward Moss

The Typologically Different Question Answering Dataset

Edward Moss (amezaliwa tar. 11 Julai 1977) ni mwigizaji wa filamu na mchekeshaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa kuigiza na kucheza kama hayati Michael Jackson kwenye filamu na vipindi vya TV.[1][2] Awali alikuwa anafanya katika kampuni ya McDonald's mwanzoni mwa miaka ya 1990, ambapo wafanyakazi wenzake walikuwa wakimwambia kama anafanana sana na mwimbaji Michael Jackson; hivyo basi Moss akaingia katika shindano la kutafuta watu wenye vipaji na kubahatika kushinda, na kadiri muda unavyokwenda, ameamua kujitafutia riziki yake kwa kujifanya kama Jackson.